Wanaanga wa SpaceX warejea: Chombo cha Dragon chatua duniani

Wanaanga wawili wa Marekani wametua huku chombo cha kwanza kufadhiliwa na kampuni binafsi kikiwasili duniani kutoka Kituo cha Anga cha Kimataifa.

Chombo cha anga cha Dragon kinachomilikiwa na kampuni ya SpaceX kilichokuwa kimewabeba Doug Hurley na Bob Behnken kilifika duniani katika ghuba ya Mexico kusini tu mwa Pensacola ghuba ya pwani ya Florida.
Hii ni mara kwanza timu iliyokwenda anga za mbali kuwasili katika bahari ya Marekani tangu wakati wa chombo cha Apollo miaka 45 iliyopita.
Waliofika kwa maboti ya kibinafsi yaliokuwa karibu na chombo cha Dragon waliombwa kuondoka huku kukiwa na wasiwasi wa kemikali hatari kutoka kwenye chombo hicho.
Afisa wa utawala wa Nasa Jim Bridenstine amesema uwepo wa boti hizo "hakikuwa kile tunachotarajia".
"Cha kushangaza ni kwamba watu ambao hawakutarajiwa waliwasili katika eneo ambalo wawili hao walitua chenye kemikali ya nitrogen tetroxide, hilo sio jambo zuri," amesema.
Picha za boti hizo zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii
"Ni heshima na farahi kwetu," amesema Hurley wakati mwanaanga huyo anawasili nyumbani.
"Kwa niaba ya chombo cha SpaceX na timu ya Nasa, karibuni tena duniani. Asante kwa kusafiri hadi anga la mbali," Timu ya SpaceX imeandika.
Rais Donald Trump - aliyehudhuria hafla ya kuzinduliwa kwa chombo hicho miezi miwili iliyopita - alipongeza kurejea kwa ujumbe huo salama.
"Asanteni nyote!" aliandika kwenye mtandao wa Twitter. "Ni furaha sana kurejea kwa wanaanga wa NASA duniani baada ya safari ya miezi miwili iliyokuwa salama."


EmoticonEmoticon