Yafahamu Madhara 11 Makubwa Ya Kuchora Tattoo Mwilini

Tattoo ni uwekaji wa wino kwenye ngozi ya ndani kitaalamu kama dermis kubadilisha rangi kabisa maisha yako yote au kwa muda tu, inateemea na uwekaji..

Madhara Ya Tattoo

1. Kansa ya ngozi

Hapo mwanzoni wataalamu walikua wanasema hakuna mahusiano kati ya kansa ya ngozi na na tabia ya kujichora tattoo lakini hivi karibuni tafiti kutoka uingereza zinaonyesha kuna aina fulani za wino ambazo zinaweza kusababisha kansa zikitumika kuchora tattoo.

2. Allergy ya Ngozi
Haijalishi unaweka tattoo kwa muda au ya moja kwa moja kumetokea kesi nyingi za watu wanaopata allergy baada ya kupakwa tattoo, utafiti unaonyesha rangi nyekundu ndio inaongoza kwa kusababisha allergy hizo huku rangi zingine kama nyeusi, purple na zingine hazisababishi.

3. Makovu
Mwili unataambua tattoo kama adui wake hivyo hujaribu kuiondoa kwa njia mbalimbali na kwa kufanya hivyo husababisha makovu ya muda mrefu ambayo yanaweza kuleta magonjwa mengine ya ngozi.

4. Maambukizi ya ukimwi na ugonjwa wa hepatitis
Tabia ya kurudia sindano zilezile wakati wa kuchora tattoo kunaweza kusababisha maambukizi ya virusi vya ukimwi na maambukizi ya virusi vinavyoshambulia ini kitaalamu kama hepatitis b. 

5. Matatizo kipindi cha kufanya kipimo cha MRI
Hichi kipimo ni cha mionzi na kirefu chake ni magnetic resonance imaging, hutumika kupima viungo vya mwili ambavyo havionekani kwa macho ndani ya mwili wa binadamu kama x ray inavyofanya.

6. Kubadilika kwa ngozi ya rangi
Sehemu inayochorwa tattoo hubadilika moja kwa moja na kua na rangi tofauti, hakuna jinsi unaweza ukaitoa hiyo rangi tena, hata baada ya muda mrefu tattoo ikipungua nguvu lakini ngozi haiwezi kua kama zamani.

7. Hutaruhusiwa kuchangia damu
Mara nyingi watu wenye tattoo hawaruhusiwi kuchangia damu kwani wana hatari ya kusambaza ugonjwa kwenda kwa mtu mwingine, kimsingi mtu aliyechora ndani ya muda mfupi ndio haruhusiwi lakini kwasababu wakati mwingine sio rahisi kutofautisha tattoo mpya na ya zamani basi hawa watu huwa hawaruhusiwi kabisa.mchezaji wa kimataifa christian ronaldo hachori tattoo kwa sababu ya hili.

8. Unaweza kukosa fursa mbalimbali
Kuna kampuni mbalimbali duniani haziwapi watu kazi kwasababu wamechora tattoo kulingana na imani za kampuni husika lakini pia kazi yeyote ya jeshi duniani hairuhusu tattoo hivyo kama wewe unayesoma hapa umeshachora tattoo ujue kazi ya jeshi huna tena.

9. Tattoo huingiliana na matumizi ya dawa Fulani
Kama wewe unatumia dawa za kuzuia damu isingane mwilini ukichora tattoo inaweza kufanya utoke damu nyingi sana kwani dawa hizo huzuia uwezo wa mwili kukausha damu na kuponyesha vidonda.

10. Magonjwa ya Ngozi
Wakati mwingine bacteria huweza kuvamia sehemu zenye vidonda vya tattoo na kusababisha kutopona haraka, dalili huweza kua homa kali, maunivu makali na sehemu ya tattoo kuvimba.

11. Damu kuganda juu ya ngozi[haematoma]
Hii husababishwa na kuvuja kwa damu nyingi chini ya ngozi, huonekana sana pembeni pembeni ya sehemu ambapo rangi ya tatoo imepita na huchelewesha kupona kwa kidonda.


EmoticonEmoticon