Zidane Afunguka Sababu Za Bale Kutocheza Mechi Ya Kufuzu Robo Fainali

Gareth Bale hakutaka kucheza katika mechi ya marudio ya kufuzu kwa robo fainali ya klabu bingwa Ulaya katika mechi dhidi ya Manchester City , kulingana na kocha mkuu wa klabu ya Real Madrid Zinedine Zidane.

Mshambuliaji wa Wales Bale aliachwa nje ya kikosi cha wachezaji 24 katika mechi ambayo timu yake ilipoteza kwa jumla ya magoli 2-1 dhidi ya klabu hiyo ya England siku ya Alhamisi usiku.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 alianza mechi 14 katika mashindano yote msimu wa 2019-20 na amecheza mara mbili tangu kandanda kurudi nchini Uhispania mwezi Juni.

''Yalikuwa mazungumzo binafsi nbaina yetu. Aliamua kutocheza'', alisema Zidane. Yaliyosalia ni kati yangu na yeye lakini ni kwamba alisema asingependelea kucheza.


EmoticonEmoticon