Aliyepigwa Risasi 7 Na Polisi Apata Fahamu Na Kutuma Video Akiwa Hospitalini, Ameongea Haya (VIDEO)

Jacob Blake, mwanaume mweusi ambaye alipigwa risasi mara saba na polisi mzungu katika jimbo la Wisconsin nchini Marekani mwezi uliopita, amesema ana maumivu yaisiyoisha katika video aliyotuma kwenye mtandao. 

Bwana Blake, ambaye familia yake inasema anaweza kupooza kuanzia sehemu ya kiuno, pia alitoa ujumbe wa matumaini, akisema kuna "mengi ya kunifanya niishi ".

Katika video iliyotumwa kwenye mtandao wa Twitter na wakiili wa familia yake, Bwana Blake-bado anaonekana akiwa kwenye kitanda cha hospitali-akizungumzia juu ya maumivu anayoyapata.

"Kila saa 24 ni maumivu, hakuna lolote ila maumivu. Inaumiza kupumua, inaumiza kulala, inaumiza kugeuka upande mmoja kuelekea mwingine, inaumiza kula ," alisema.
"Maisha yako, na sio maisha yako tu, miguu yako, kitu unachokihitaji utembee na kuendeleza maisha, vinaweza kuchukuliwa kama hivi ," alisema, huku akigongesha vidole vyake.

"Muwe na umoja , tengenezeni pesa, fanya mambo kuwa rahisi kwa watu wetu, kwasababu kuna muda mwingi ambao umepotezwa ," aliongeza


EmoticonEmoticon