Aliyevamia Nyumbani Kwa Rapa Eminem Amethibitisha Alikuwa Anataka Kumuua

Kesi ya Mvamizi aliyeingia kwenye nyumba ya Eminem mwezi April mwaka huu imeanza kusikilizwa, imewekwa wazi kwamba alifika pale kwa ajili ya kumuua Eminem.

Kwa mujibu taarifa za kiuchunguzi, Matthew David Hughes (27) aliingia nyumbani Eminem kwa kupitia dirisha ambalo lilikuwa limevunjika.

Baada ya Eminem kuamka siku hiyo ya April 5, alijikuta akiwa amesimamiwa na mtu kwa nyuma. 

Kwa haraka aliamini ni mpwa wake kabla ya kugundua kwamba ni mvamizi, amesema Afisa Adam Hackstock mbele ya mahakama ambapo alithiibitishia mahakama pia kwamba baada ya kumbana Matthew, alisema kwamba alifika pale kwa ajili ya kumuua rapa huyo.

Matthew amekuwa akishikiliwa tangu kutokea kwa tukio na dhamana yake ilitajwa kuwa ni pesa taslimu ($50,000) na alishtakiwa kwa kosa la kwanza la uvamizi wa nyumbani na uharibu wa mali kwa kukusudia.


EmoticonEmoticon