Android 11 Yazinduliwa Rasmi, Fahamu Maboresho Matano Muhimu

Watumiaji wa aina mbalimbali za simu zinazotumia mfumo wa Android wiki hii wataanza kupata Android 11.

𝗔𝗻𝗱𝗿𝗼𝗶𝗱 𝟭𝟭 𝗶𝘁𝗮𝗸𝘂𝘄𝗮 𝗻𝗮 𝗳𝗲𝗮𝘁𝘂𝗿𝗲𝘀 𝘇𝗶𝗳𝘂𝗮𝘁𝗮𝘇𝗼:
1. Android imeamua kuweka mfumo wa Bubble Messages ili kurahisisha watumiaji wa Android kuweza kufungua app na kujibu messages kwa pamoja. Ni style ambayo ilikuwa inatumia zamani na Facebook Messenger, ambapo app hiyo ilikuwa inaweza kutokea katika screen, ukaona conversation na kuijibu hata ukiwa umefungua app nyingine

2. Google ameboresha mpangilio wa mijadala (Conversations) katika notifications na sehemu ya messages kuweka urahisi wa kusoma message na kufuatilia mijadala katika apps za kuchati.

3. Sehemu ya juu katika “Control” imefanyiwa maboresho ya muonekano. Android 11 ina mpangilio mzuri na muonekano mzuri kuweka urahisi wa kutumia Control Center katika kuwasha Bluetooth, kubadili mziki au kubadilisha mwanga wa simu, pia kuna sehemu na app maalum katika kutumia vifaa vya wireless.


4. Android 11 ina speed katika kuunganisha vifaa vinavyotumia bluetooth kama speakers na imekuwa rahisi kuunganisha vifaa mbalimbali kwa pamoja katika setting mpya. Hii ni style ambayo wameichukua katika iOS.


5. Ina maboresho katika kupiga screenshot na kurekodi screen yako. Android imeweka uwezo wa ku-pause, tofauti na iOS ambayo screen record haiwezi ku-pause.


Unaweza kushare mziki katika wireless speakers au headphones kwa pamoja.


EmoticonEmoticon