Baada Ya Kupewa Sumu, Hatimaye Mkosoaji Mkuu Wa Rais Vladimir Putin Wa Urusi Apata Fahamu

Madaktari waliokuwa wakimtibu kiongozi wa upinzani nchini Urusi Alexei Navalny wanasema kwamba amepata fahamu na kwamba hali yake tangu alipopatiwa sumu imeimarika.

Amekuwa akijibu anachoulizwa . Bwana Navalny , mwenye umri wa miaka 44 alisafirishwa hadi nchini Ujerumani baada ya kuugua katika ndege moja huko Siberia mwezi Agosti.
Wasaidizi wake wanadai kwamba alipatiwa sumu kufuatia agizio la rais Vladmr Putin ambaye amekana kuhusika na suala hilo.
Madaktari wa Ujerumani wanasema kwamba mkosoaji huyo wa rais Putin alipatia sumu ya Novichok .

Siku ya Jumatatu hopsitali ya Charite iliopo mjini Berlin ilisema katika taarifa kwamba bwana Navalny alikuwa anaondolewa polepole mashine inayomsadia kupumua, hatahivyo bado ni mapema sana kupima athari za baadaye za sumu hiyo, ilisema.
Madaktari pia walisema kwamba wanawasiliana mara kwa mara na mke wa Navalny.
Msemaji wa Navalny , Kira Yarmsh , alituma ujumbe wa twitter akisema habari kuhusu Alexei. Leo amepata fahamu .
Atandolewa pole pole katika mashine inayomsadia kupumua. Anajibu anapozungumziwa . Bwana Navalny ni mwanaharakati dhidi ya ufisadi ambaye katika miaka ya hivi karibuni amekuwa kiongozi maarufu wa upinzani nchini Urusi.


EmoticonEmoticon