Baada Ya Kusubiriwa Kwa Muda Mrefu, Hatimaye Tarehe Kamili Ya Kutoka Kwa Documentary Ya Rihanna Yawekwa Wazi

Documentary ya Rihanna ambayo imekuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu sasa kuachiwa mwaka 2021.

Muongozaji wa Documentary hiyo, Peter Berg ameweka wazi kwamba kazi hiyo itapatikana kwenye mtandao wa Amazon kuanzia mwezi Julai mwaka 2021.

"Documentary ya Rihanna ni kitu ambacho nimekuwa nikikifanyia kazi pamoja naye kwa takribani miaka 4 sasa, Amazon wataiachia kwenye msimu wa majira ya Joto mwaka 2021, kwenye tarehe za kama Julai 4 hivi. imekuwa safari ndefu sana kwa miaka 4." alisema Muongozaji Peter.

Huwenda tungeipata mapema, Muongozaji huyo amesema Documentary hiyo imechelewa kutokana na ratiba ngumu za Rihanna na biashara zake.


EmoticonEmoticon