Baba Mzazi Wa Bilionea Bill Gates Afariki Dunia

Baba Mzazi wa Bilionea Bill Gates, William Henry Gates II amefariki akiwa na miaka 94, familia haijatoa chanzo cha kifo chake lakini itamkumbuka kwa mengi ikiwemo kuwa miongoni mwa Waanzilishi The Bill & Melinda Gates Foundation.

Foundation hiyo ya The Bill & Melinda Gates imekua ikitoa misaada kwa Nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania na hata Bill Gates mwenyewe ameonesha mapenzi na Tanzania ambapo mara ya mwisho alikuja na kufika hadi Muheza Tanga.


EmoticonEmoticon