Baba Wa Messi Ashuka Barcelona Kufanya Mazungumzo Ya Mwanae Kuondoka Barcelona

Baba yake Lionel Messi na wakala wake, Jorge, wamekutana na rais wa Barcelona Josep Maria Bartomeu, aliyesema kwamba klabu hiyo haitafanya mazungumzo ya kumuuza mshambuliaji huyo wa Argentina, 33.

Mkutano wa kwanza tangu Messi kutoa ombi la kuondoka klabu hiyo ukiishia bila makubaliano huku Barcelona ikisema ofa ya miaka miwili kwa mchezaji huyo bado ipo.
Kima cha malipo ili Messi aruhusiwe kuondoka Barcelona huenda kikawa kidogo pengine hata euro milioni 100.


EmoticonEmoticon