BET Watangaza Majina Ya Wanaowania Tuzo Hizo Mwaka 2020

September 29 - BET walitangaza vipengele 17 vya tuzo za 15 za (BET Hip Hop Awards), ambazo zimetajwa kuoneshwa Oktoba 27 mwaka huu. 

Kinda DaBaby ambaye mwaka 2019 aling'ara kwa kupita na tuzo ya Msanii Bora wa Hip Hop Chipukizi, ameongoza kwa kutajwa kwenye vipengele vya tuzo za mwaka huu, akitajwa kwenye vipengele 12 akifuatiwa na Roddy Ricch mwenye vipengele 11. 

Megan Thee Stallion amefungana na mastaa wa dunia kama Drake wakiwa na vipengele 8 kila mmoja. Wengine ni Beyonce, DJ Khaled, Travis Scott, Mustard ambao wametajwa kwenye vipengele 3 kila mmoja. 

Habari njema ni kwamba Afrika Mashariki imepata mwakilishi kwenye tuzo za mwaka huu, ni rapa Khaligrah Jones toka Kenya ambaye ametajwa kwenye kipengele cha 'Best International Flow' akichuana na wakali toka Ufaransa, Uingereza, Brazil na Afrika Kusini inayowakilishwa na Nasty C.


EmoticonEmoticon