Cardi B Aitaka Talaka, Huku Mahakama Ikiwakilishiwa Maombi Ya Haki Ya Malezi Ya Mtoto Wao

Cardi B ameamua kumalizana na Offset kabisa. Baada ya taarifa za kuitaka talaka kutoka usiku wa kuamkia leo, kuna mengi yameibuka toka kwenye shauri hilo.

Tovuuti ya XXL imeripoti kwamba, nyaraka zilizowasilishwa Mahakama Kuu ya kitongoji cha Fulton mjini Georgia zinaeleza kwamba, Cardi B anataka haki ya muda wote (Full Custody) ya malezi ya mtoto wao Kulture Kiari Cephus. Hataki kabisa Offset apate angalau nafasi ya kukaa na binti huyo mwenye umri wa miaka 2 sasa.

Mbali na kutaka haki ya kumlea Kulture peke yake, Cardi B pia ameomba huduma ya matunzo ya mtoto yaani Child Support toka kwa Offset.


EmoticonEmoticon