Cardi B Mwenyewe Ametoa Sababu Za Kuitaka Talaka Toka Kwa Mume Wake Offset

Mwanzoni mwa wiki iliyoisha tuliripoti kuhusu madai ya rapa CardiB kwenda mahakamani na kufungua 'file' la kudai talaka kutoka kwa mumewe ambaye ni msanii wa kundi la Migos, Offset.

Sasa kama ulikuwa unafikiri kwamba 
CardiB kuachana na Offset ni kwa sababu ya matukio ya usaliti kipindi cha nyuma, basi fahamu kwamba sio kweli.

Kupitia IG LIVE mwishoni mwa wiki, 
CardiB alikanusha stori hizo, akisema ameamua kukaa mbali na ndoa hiyo kwa sababu anaogopa kuja kupigwa matukio ya usaliti siku za usoni kwa kile alichodai kwamba kuna mambo yanaendelea kwa Offset ambayo hafurahishwi nayo.

"Nimechoka na kila siku kubishana, nimechoka na kutoshuhudia vitu kwa macho. Pale unapohisi kwamba haipo sawa tena. Kabla ya kusalitiwa, ni bora kuondoka." alizungumza Cardi B.


EmoticonEmoticon