Chanjo Ya Urusi Yaonesha Dalili Za Kukabiliana Na Virusi

Wanasayansi wa Urusi wamechapisha taarifa ya kwanza juu ya chanjo yao ya virusi vya corona, wakisema kuwa vipimo vya awali vimeonesha ishara ya chanjo hiyo ya kuuwezesha mfumo wa kinga ya mwili kupambana na virusi.

Ripoti iliyochapishwa na jarida la kitabibu la The Lancet ilisema kuwa kila mshiriki aliyepewa chanjo hiyo aliweza kutengeneza sehemu ya protini ya damu inayoweza kuua virusi, bakteria na vimelea wengine hatari wanaoshambulia mwili wa binadamu(Antibodies) na haikuwa na athari mbaya.
Urusi iliidhinisha chanjo hiyo kutumiwa ndani ya nchi mwezi Agosti, ikiwa ni nchi ya kwanza duniani kufanya hivyo kabla ya kuchapishwa kwa data juu ya ufanisi wa chanjo.
Wataalamu wanasema majaribio yalikuwa ni madogo sana kuweza kuidhinisha ufanisi na usalama wa chanjo hiyo.
Lakini utawala wa Moscow umesifu matokeo ya chanjo yao na kuyataja kama jibu kwa wakosoaji.
Baadhi ya wataalamu wa nchi za magharibi wameelezea hofu zao juu ya kasi ya kazi ya Urusi, wakisema kwamba watafiti huenda walitumia njia fupi kutengeneza chanjo hiyo.
Mwezi uliopita Rais Vradimir Putin alisema kwamba chanjo hiyo imepita vigezo vyote vya uchunguzi na mmoja wa watoto wake wa kike alipewa chanjo hiyo.


EmoticonEmoticon