Diamond Platnumz Ashirikishwa Kwenye Album Ya Alicia Keys Toka Marekani

Malkia wa Muziki tokea nchini Marekani Aliciakeys , ameachia Rasmi ‘Track List’ ya Nyimbo ambazo zitapatikana kwenye Album yake ya ALICIA ambayo anatarajia kuiachia siku ya Kesho Ijumaa , September 18 .

Album hiyo ina Jumla ya Ngoma 15 , huku Nyimbo Namba 4 WastedEnergy akiwa amemshirikisha Star wa Muziki tokea barani Afrika Diamond Platnumz .
Diamond ameandika Historia Nyingine katika Muziki wa Tanzania na Afrika kwa ujumla , Kutokana na Ukubwa na Ushawishi alionao Aliciakeys kwenye Muziki Duniani.

Hii inaweza kuwa nafasi kubwa sasa ya Muziki wa Tanzania kutiliwa umaanani zaidi nchini Marekani na Duniani kwa ujumla , Pia nafasi kubwa ya kuweza kupata nafasi ya kuwa ‘nominated’ Kwenye Tuzo kubwa kama Grammy .

Album ya “ALICIA “ itakuwa Album ya 13 Kutoka Kwa Aliciakeys na Album ya Kwanza ndani ya Miaka 3 , tangu alivyoachia Album yake ya Mwisho “Dirty Dancing 2” Mwaka 2017 .


EmoticonEmoticon