Facebook Waifungia Akaunti Ya Aliyetaka Kuonyesha Live Akikata Roho

Facebook imetangaza kuifungia kwa muda akaunti ya Raia wa Ufaransa Alain Cocq(57) ambaye ametangaza kuwa ataruka LIVE Facebook wakati akiwa anakata roho, Alain amepanga kufanya hivyo ili kupaza sauti kuhusu umuhimu wa Ufaransa kutunga Sheria inayoruhusu Mgonjwa ambaye ameteseka sana kwa maradhi kupewa dawa ili afe.

Alain alimuomba Rais Emmanuel Macron aruhusu Madaktari wampe dawa itakayoondoa uhai wake kutokana na kuugua kwa muda mrefu lakini Rais alikataa akisema Sheria za Nchi haziruhusu> "nimeacha kula, kunywa na kutumia dawa nitafariki siku sio nyingi na nitarusha LIVE nikiwa nakata roho"

Facebook imesema tukio hilo ni kinyume na kanuni zao na hawatoruhusu liende LIVE hivyo wanaifunga akaunti, Alain ameugua muda mrefu kufuatia kuungana kwa mishipa yake ya damu inayotoka kwenye moyo.


EmoticonEmoticon