Kampuni
ya Facebook imeshtakiwa kwa tuhuma za kuwafuatilia watuamiaji wa Instagram kwa
kutumia kamera za simu zao bila ridhaa ya watumiaji.
Kesi hiyo imetokana na ripoti za vyombo vya habari kuwa
mtandao huo wa kushirikishana picha umekuwa ukitumia kamera za simu za iPhone
hata pale ambapo watumiaji wa simu hizo hawatumii kamera.
Facebook imekanusha tuhuma hizo na kueleza kuwa kulikuwa na
hitilafu ya programu (bug) ambayo inairekebisha.
Imesema kuwa ‘bug’ hiyo ilikuwa ikitoa taarifa (notification) kwa watumiaji
wa Instagram kuwa iPhone inatumia kamera zao, jambo ambalo halikuwa kweli.
Katika kesi hiyo iliyofunguliwa New Jersey, Marekani,
mtumiaji wa Instagram ambaye ni mlalamikaji, Brittany Conditi, amesema kuwa
programu hiyo (Facebook) inatumia kamera za iPhone kwa makusudi ili kukusanya
taarifa za siri watumiaji ambazo hawawezi kuzikusanya kwa njia nyingine.
Katika kesi nyingine iliyofunguliwa mwezi uliopita Facebook
ilituhumiwa kutumia teknolojia ya utambuzi wa sura (facial-recognition) kukusanya
taarifa (biometric data) za
watumiaji wa Instagram zaidi ya milioni 100 kinyume na sheria. Hata hivyo
kampuni hiyo ilikanusha madai hayo kwa maelezo kuwa Instagram haitumii
teknolojia hiyo.
EmoticonEmoticon