Habari 5 Kubwa Za Soka Ulaya Alhamisi September 10

Tetesi Za Soka Ulaya Alhamisi September 10

1. Barcelona imewasiliana na Arsenal kuhusu uhamisho wa beki wa kulia Mhispania Hector Bellerin, 25. Mabingwa wa Ufaransa Paris St-Germain pia wanamtaka Bellerin na imeshawasiliana na wawakilishi wake.

2. Manchester United imekamilisha usajili wa mshambuliaji Alejandro Garnacho,16, kutoka Atletico Madrid. Kinda huyo atawasili kutoka Hipsania baadae wiki hii, na atapaswa kukaa karantini kwa siku 14.

3. Real Madrid wako tayari kulipa nusu ya mshahara wa mwaka wa Gareth Bale ili kusaidia mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 31 raia wa Wales kuondoka katika timu hiyo ya Hispania. 

4. Mshambuliaji wa Everton na Italia Moise Kean, 20, anataka kurudi Juventus, klabu aliyotoka kabla ya kijuiunga na Toffees mwaka 2019.

5. Bournemouth wanataka kumsainisha kiungo wa pembeni wa Scotland na Newcastle Matt Richie lakini wamekwama kukubaliana na masharti binafsi ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30.


EmoticonEmoticon