Habari 5 Kubwa Za Soka Ulaya Alhamisi September 17

Tetesi Za Soka Ulaya Alhamisi September 17

1. Mlinzi wa kushoto wa Real Madrid na Uhispania Sergio Reguilon ,23, yupo katika kiwanja cha mazoezi cha Tottenham kwa vipimo vya afya kabla ya kujiunga na klabu hiyo ya ligi kuu.

2. Kocha wa Everton Carlo Ancelotti anataka kumsajili mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa Chelsea Fikayo Tomori, 22, lakini pia yuko tayari kuwaachia wachezaji kadhaa akiwemo viungo wa kati Gylfi Sigurdsson, 31, na Fabian Delph , 30 .
3. Manchester City wanajiandaa kuwa uhamisho wa mchezaji wa nafasi ya ulinzi anayekipiga Atletico Madrid, Jose Gimenez, ikiwa Napoli itakataa kushusha dau kwa ajili ya mlinzi wa kati Kalidou Koulibaly,29.
4. Kiungo mkabaji wa Atletico Madrid Thomas Partey,27, ni miongoni mwa wachezaji wanaolengwa na Arsenal lakini klabu hiyo ya Uhispania watamuuza tu iwapo dau la pauni milioni 45 litafikiwa.
5. Kocha wa Barcelona Ronald Koeaman amesema kuwa timu hiyo haitamrejesha mlinzi wa Manchester City, Mhispania Eric Garcia,19. 


EmoticonEmoticon