Habari 5 Kubwa Za Soka Ulaya Jumanne September 1

Tetesi Za Soka Ulaya Jumanne September 1, 2020

1. Chelsea imekubali kumsajili kiungo wa kati wa Bayer Leverkusen na Ujerumani Kai Havertz, 21, kwa kima cha kwanza cha pauni milioni 72, na kusababisha pesa za matumizi yao kipindi cha uhamisho kuongezeka hadi pauni milioni 200. 

2. Kiungo wa kati wa Uhispania Dani Ceballos, 24, anasemekana kwamba wiki hii atajiunga na Arsenal kwa mkopo kutoka Real Madrid.

3. Tottenham imeanzisha mazungumzo ya mkataba mpya wa mlinda lango wa Ufaransa Hugo Lloris, 33, licha ya kumsajili Joe Hart kwa uhamisho wa bure.

4. Arsenal imekubali kumtoa beki wa kati Rob Holding, 24, Newcastle United kwa mkopo na makubaliano hayo yanatarajiwa kukamilika wiki hii.

5. Manchester United inamlenga mlinzi wa RB Leipzig raia wa Ufaransa Dayot Upamecano, 21. 


EmoticonEmoticon