Habari 5 Kubwa Za Soka Ulaya Jumanne September 16

Tetesi Za Soka Ulaya Jumanne September 16

1. Tottenham huenda wakamtumia kiungo wa kati wa England Dele Alli, 24, chambo wakati wakijaribu kumrejesha Gareth Bale, 31, kutoka Real Madrid.

2. Arsenal bado wanapanga kuwaongeza wachezaji zaidi kwenye kikosi chao, huku wakiwalenga kiungo wa kati wa Atletico Madrid Thomas Partey, 27 na kiungo mchezeshaji wa Lyon, Mfaransa Houssem Aouar,22, miongoni mwa wachezaji wanaowataka.

3. Barcelona itajaribu kumsajili mchezaji wa nafasi ya ulinzi anayekipiga Manchester City Eric Garcia,19, msimu huu ikiwa wataweza kuwauza walinzi wa kati Samuel Umtiti,26, na Jean-Clair Todibo,20. 

4. Juventus wanakumbana na wakati mgumu kuhusu kumsajili mshambuliaji wa Barcelona Luis Suarez, ambaye anapata changamoto kupata pasi ya Italia kwa haraka.

5. Bayern Munich wako tayari kurudisha shauku yao kwa ajili ya winga Callum Hudson-Odoi, 19, huku wababe hao wa ligi ya mabingwa Ulaya wakiwa na matumaini kuwa Chelsea itapokea ofa yao.


EmoticonEmoticon