Habari 5 Kubwa Za Soka Ulaya Jumanne September 8

Tetesi Za Soka Ulaya Jumanne September 8

1. Man United inatumai kuwasajili wachezaji watatu kabla ya kukamilika kwa dirisha la uhamisho la msimu huu, huku mshambuliaji wa England na Borussia Dortmund Jadon Sancho 20 akisalia mchezaji wanayemlenga kwa udi na uvumba.

2. Uwezo wa mkufunzi wa Real Madrid Zinedine Zidane kukibadilisha kikosi chake kutategemea iwapo Man United itamsajili mshambuliaji wake Gareth Bale. 

3. Klabu za ligi ya Premia zinaamini kwamba Brewster ataruhusiwa kuondoka Liverpool katika dirisha hili la mismu wa uhamisho huku klabu za Sheffield United na Crystal Palace pia zikiwa na hamu ya kumsajili mshambuliaji. 

4. Barcelona ina hamu ya kumsajili kiungo wa kati wa Bayern Munich na Uhispania Thiago Alcantara, 29 - ambaye analengwa na Liverpool kurudi katika klabu hiyo. 

5. West Ham imejiandaa kutoa dau lililoimarika la £30m kumnunua beki wa Burnley na England James Tarkowski, 27.
Hatahivyo, Burnley inataka £50m iwapo watalazimika kumuuza mchezaji huyo wa England


EmoticonEmoticon