Habari 5 Kubwa Za Soka Ulaya September 3

Tetesi Za Soka Ulaya Alhamisi September 3, 2020

1. Kocha mpya wa Barcelona Ronald Koeman anataka klabu hiyo kufanya kila linaloweza kumsajili kiungo wa kati wa Liverpool na Uholanzi Georginio Wijnaldum, 29.

2. Paris St-Germain imepunguza fursa ya uwezekano wa kumsajili kiungo wa kati wa Ufaransa, Matteo Guendouzi, 21, kutoka Arsenal.

3. DC United imechukua hatua ya kumtafuta mshambuliaji wa Juventus Gonzalo Higuain, 32, na pia inamnyatia kiungo wa kati wa Everton kutoka Iceland, Gylfi Sigurdsson, 30. 

4. Manchester United imealikwa katika majadiliano na Bayern Munich kuhusu kiungo wa kati Thiago Alcantara, 29. 

5. Washambuliaji wa Arsenal Ainsley Maitland-Niles na Kieran Tierney, wote wakiwa na umri wa miaka 23, watasalia klabu hiyo baada ya kocha Mikel Arteta kusema wazi kwamba anataka wawe sehemu ya kikosi chake.


EmoticonEmoticon