Habari 5 Kubwa Za Soka Ulaya September 18

Tetesi Za Soka Ulaya Ijumaa September 18

1. West Brom wanajaribu kumsajili mshambuliaji wa Aston Villa, Mbwana Samatta, kabla ya mchezaji huyo mwenye miaka 27, hajamaliza mchakato wa kuhamia Fenerbahce.

2. Liverpool wamemfuatilia Ismaila Sarr na kujadili suala lake na Watford, ambayo inataka pauni milioni 36 kwa ajili ya mshambuliaji huyo.

3. Sarr pia ametambulika na Manchester United kama mbadala ikiwa mpango wa kumnasa winga wa Borussia Dortmund Jadon Sancho utashindwa.

4. Wakala wa Edouard Mendy amedai kuwa makubaliano yameafikiwa kwa ajili ya mlinda mlango huyo, 28, anayekipiga katika klabu ya Rennes kujiunga na Chelsea.

5. West Ham imebadili muundo wa ofa kwa ajili ya kumnasa Tarkowski lakini ofa hiyo bado imekataliwa na Burnley.


EmoticonEmoticon