Habari Kubwa 5 Za Soka Ulaya Ijumaa September 4

Tetesi Za Soka Ulaya Ijumaa September 4, 2020

1. Baba yake Lionel Messi amejadiliana na Barcelona kwa siku ya pili mfululizo juu ya uwezekano wa kijana wake kuhama klabu hiyo, na mlinzi wa Liverpool Andy Robertson anasema ni matumaini yake kwamba mshambuliaji huyo, 33, wa Argentina hatasajiliwa na timu nyingine ya ligi ya primia.

2. Rais wa Napoli Aurelio de Laurentiis amesema wanataka kumsajili mlinzi wa Arsenal ,Mgiriki, 32, Sokratis Papastathopoulos, hatua ambayo inaweza kutoa mwaya kwa Kalidou Koulibaly, 29, kujiunga na Manchester City. 

3. Mlinzi wa Manchester United Chris Smalling, 30, anaonekana kuwa tayari kujiunga na Roma kwa mkataba wa kudumu. 

4. Manchester United inajaribu kumaliza suala la mshahara na kima cha uhamisho kwa winga wa Borussia Dortmund Jadon Sancho kabla ya kutoa ofa kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa England.

5. Sevilla ina matumaini ya kuendelea kuwa na beki wa Real Madrid Sergio Reguilon kwa mkopo kwa msimu mwingine licha ya Mhispania huyo, 23, kuhusishwa na uhamisho wa kudumu hadi Manchester United.


EmoticonEmoticon