Habari Kubwa Za Soka Ulaya Jumatano September 2

Tetesi Za Soka Ulaya Jumatano September 2, 2020

1. Juventus inataka kumsajili mshambuliaji wa Barcelona na Uruguay Luis Suarez, 33, au wa Roma, Bosnia Edin Dzeko, 34.

2. Paris St-Germain imeahidi kutoa pauni milioni 25 pamoja na pauni milioni 5 za ziada-kwa beki wa kulia wa Arsenal Hector Bellerin, huku Bayern Munich na Juventus pia zikionesha nia ya Kumsajili mlinzi huyo wa Uhispania, 25. 

3. Chelsea imesema thamani ya N'Golo Kante ni pauni milioni 80 huku Inter Milan ikionesha nia ya kumsajili kiungo huyo wa kati wa Ufaransa, 29. 

4. Kocha wa Tottenham Jose Mourinho yuko tayari kumuuza kiungo wa kati wa Ufaransa Tanguy Ndombele, 23 ambaye usajili wake uliweka historia.

5. Newcastle inajaribu kufikia makubaliano ya Callum Wilson, 28, wa Bournemouth ambayo yatamuwezesha winga wa Scotland Matt Ritchie kujiunga na Cherries, lakini Aston Villa pia inamnyatia mshambuliaji huyo wa England.


EmoticonEmoticon