Habari Kubwa Za Soka Ulaya Jumatatu September 7

Tetesi Za Soka Ulaya Jumatatu September 7

1. Mkufunzi mpya wa Barcelona Ronald Koeman ameambia klabu hiyo anataka kumzuia Phillipe Coutinho msimu huu badala ya kumtoa mchezaji huyo wa Brazil kwa mkopo.

2. Mkufunzi wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amezungumza na winga wa England Jadon Sancho, 20, kuhusu kujiunga na klabu hiyo kutoka klabu ya Borussia Dortmund msimu huu.

3. Licha ya Gareth Bale kutaka kuondoka Real Madrid , klabu hiyo haijapokea maombi yoyote ya mshambuliaji huyo wa Wales, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 akikataa kupunguziwa mshahara wake na hivyobasi kuwazima wanaommezea mate.

4. Mshambuliaji wa Barcelona Luis Suarez, 33, anatarajiwa kukalia mtihani wa Lugha siku ya Jumatatu ili kupatiwa uraia wa Itali , hatua itakayomfanya kukamilisha uhamisho wake kujiunga na Juventus.

5. West Ham italazimika kuongeza ombi lao la dau la £27m ili kuwa na fursa yoyote ya kumsajili beki wa kati wa Burnley James Tarkowski, 27.


EmoticonEmoticon