Habari Kubwa Za Soka Ulaya Jumatatu September 14

Tetesi Za Soka Ulaya Jumatatu September 14

1. Manchester United itapaswa kulipa kiasi cha pauni milioni 18.5 pekee ikiwa wanataka kumsajili winga wa Real Madrid na Wales Gareth Bale, 31.

2. Douglas Costa amewekwa tayari kuuzwa na Juventus. Manchester United awali walikuwa wakihusishwa na taarifa za kumtaka winga huyo wa Brazil, 29.

3. Arsenal inataka kumsajili mlinda mlango wa Iceland Rinar Runarsson, 25, na imeanza mazungumzo na Dijon kuhusu mpango huo.

4. Tottenham inaweza kuchuana na Manchester United kupata saini ya Beki wa kushoto wa Real Madrid, Mhispania Sergio Reguilon,23.

5. Spurs wako kwenye mazungumzo na Trabzonspor kwa ajili ya mpango wa kumpata mshambuliaji Alexander Sorloth. Mchezaji huyo, 24 anacheza kwa mkopo wa miaka miwili akitoka Crystal Palace.


EmoticonEmoticon