Habari Tano Kubwa Za Soka Ulaya Ijumaa September 11

Tetesi Za Soka Ulaya Ijumaa September 11

1. Mshambuliaji wa Tanzania, Mbwana Samatta, 27, ataweza kuondoka Aston Villa miezi minane tu baada ya kujiunga na klabu hiyo. 

2. Kiungo wa Liverpool Georginio Wijnaldum, 29, amefanya mazungumzo yaliyoenda vizuri na meneja Jurgen Klopp kuhusu mustakabali wake klabuni hapo. Mholanzi huyo amebakiza mwaka mmoja kwenye kandarasi yake ya sasa pale Anfield. 

3. Kiungo wa Manchester United na Brazil Fred, 27, amepuuza ripoti kwamba anaweza kuondoka msimu huu na kujiunga Galatasaray na Uturuki. 

4. Mshambuliaji wa Arsenal na Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 31, atasaini mkataba mpya wa miaka mitatu na klabu hiyo utakaomfanya kuwa mchezaji anayelipwa zaidi klabuni hapo.

5. Chelsea imekataa ofa ya Inter Milan kwa ajili ya kiungo wake aliyetwaa kombe la dunia N'Golo Kante, 29, ofa ambayo inajumuisha kubadilishana na kiungo wa Croatia Marcelo Brozovic, 27.


EmoticonEmoticon