India Yaipiku Brazil Kwa Visa Vya Corona Yashika Nafasi Ya Pili

Leo September 7, 2020 Wizara ya Afya nchini India imetangaza ongezeko la visa vipya 90,802, idadi hiyo inaifanya India kurekodi jumla ya maambukizi 4,204,613.

India inaipiku Brazil (4,137,606) na kuwa nchi ya pili kuathirika zaidi na janga la COVID19 ulimwenguni baada ya Marekani ambayo ina visa 6,115,394.

Vilevile, Mamlaka imerekodi vifo 1,016 ikiwa ni siku ya 5 mfululizo kwa Taifa hilo kurekodi vifo zaidi ya 1,000. 

Hadi sasa India imeripoti vifo 71,687 na wagonjwa 3,250,429 wamepona.


EmoticonEmoticon