Kanye West Aitupa Tuzo Ya Grammy Chooni Na Kuikojolea

Kanye West ameitupa chooni tuzo ya Grammy na kuikojolea, tuzo ambayo ni ndoto ya kila msanii duniani kuja angalau kuishika tu kwa mikono yake. 

Kanye anafanya hivi ikiwa ni mwendelezo wake wa kutilia mkazo madai yake ya uonevu na utumwa wanaofanyiwa wasanii kwenye lebo za muziki na makampuni. 

Wiki hii Kanye amekuwa akipazia sauti suala hilo kupitia ukurasa wake wa Twitter na kuzitupia lawana lebo za Sony na Universal, na amefikia hatua ya kutaka kununua haki zote za kazi zake yaani Master Recordings toka kwenye lebo hizo. 

Kanye ni mshindi mara 21 wa tuzo za Grammy, akiwa miongoni mwa wasanii walioshinda mara nyingi zaidi. 

Akisisitiza kwamba tayari “ametengeneza mamilioni ya pesa”,  Kanye anasema yeye ni mmoja wa watu wachache wanaoweza kusema waziwazi juu ya suala hili bila kujali matokeo yake — maana yake ikiwa ni kwamba yeye ni tajiri kiasi cha kutosha kwamba hawezi kubabaika na manyanyaso ya  lebo zenye kurekodi muziki.


EmoticonEmoticon