Kiongozi Wa Kuwait Afariki Dunia

Kiongozi wa Kuwait Sheikh Sabah Al Ahmad Al Sabah amefariki dunia.Al Sabah ambaye atakumbukwa kwa juhudi za kidiplomasia za kupigia debe uhusiano wa karibu na Iraq baada ya vita vya Ghuba vya mwaka 1990, pamoja na kutafuta suluhu katika mizozo mingine ya kikanda, amekufa siku ya jana Jumanne akiwa na umri wa miaka 91.

Ukanda wa mashariki ya kati, Sheikh Sabah alisifika kwa juhudi zake za kuweka mbele diplomasia ili kusuluhisha mzozo kati ya Qatar na mataifa mengine ya Kiarabu.Al Sabah aliingia madarakani mwaka 2016, baada ya bunge kupiga kura ya kumuondoa mamlakani mtangulizi wake Sheikh Saad Al Abdullah Al Sabah, siku tisa tu katika utawala wake.

Shirika la habari linalomilikiwa na serikali lilitangaza kifo chake baada ya maombi maalum.Nafasi yake inatarajiwa kujazwa na kaka yake, mfalme Sheikh Nawaf Al Ahmad Al Sabah mwenye umri wa miaka 83.


EmoticonEmoticon