Lil Wayne Kuachia Original Album Ya Carter V

Lil Wayne
Lil Wayne kuachia toleo asili (Original Version) ya album yake "Tha Carter V" wiki ijayo. 

Dokezo hilo limetolewa na rapa Mack Maine kwenye video moja iliyosambaa ameonekana akisema wataachia album hiyo wiki ijayo kwenye majukwaa ya kusikiliza na kupakua muziki mtandaoni.

Album ya Carter V iliyotoka mwaka 2018, ilitoka kwa jasho mara baada ya Lil Wayne kuishikilia kwa takribani miaka 8 kutokana na kukosekana kwa maelewano kati yake na Birdman.

Hivi karibuni Wayne amekuwa akidokeza ujio wa album ya Tha Carter VI, na alisema ipo tayari.


EmoticonEmoticon