Limao Sio Zuri Kwa Afya Ya Uzazi Kwa Mwanaume, Wataalamu Washauri Hilo

Madaktari wanasema limau ni moja ya tunda muhimu kwa mwili wa binadamu kutokana na virutubisho vyake. 

Jarida la Healthline lililoangazia kwa kina umuhimu wa limau kwa afya linasema lina madini ya Vitamin C, ambayo yanachangia asilimia 20 ya mahitaji ya binadamu mwilini.
Pia lina madini ya chuma, calcium, vitamin B, potassium na magnesium
Utafiti unaonesha kwamba kunywa juisi ya limau kunaimarisha kinga ya mwili, kupunguza hatari ya kupata magonjwa ya moyo na figo na pia kunaimarisha afya ya ngozi.
Hajia Jummai Hassan, mshauri wa chakula bora katika hospitali ya Wuce mjini Abuja, ameiambia BBC kuwa kando na manufaa mengine kwa afya limau linasaidia katika ukuzaji wa nguvu za kiume.

Anasema Limau lina matumizi tofauti lakini pia- linatumiwa kwa juisi na chakula pia.
"Watu wanafikiria ni hatari kwa wanandoa kutumia limau lakini hiyo ni dhana potovu. Kwa sababu utafiti unaonesha kuwa matumizi kiasi ya limau yanasaidia kuimarisha nguvu za kiume."
"Kiwango kidogo cha maji ya limau kikiwekwa katika maji ya kunywa ama kwenye chai hakiwezi kuathiri nguvu za kiume - bali kinatengeneza na kuziimarisha zaidi."
"Bila Shaka najua kunywa maji ya limau nusu kikombe - ni hatari kwa afya ya uzazi wa wanaume," anasema mtaalamu huyo wa masuala ya lishe bora.

Anasema kunywa maji mengi ya limau kunaweza kudhibiti ukuzaji wa nguvu za kiume kwa wale ambao hawataki tena kupata watoto.
Pia ameongezea kuwa utafiti uliofanywa nchini Australia umeonesha kuwa kunywa maji ya limau kwa wingi kunaweza kuathiri nguvu za kiume.
"Endapo utatumia maji ya limau kabla ya kufanya tendo la ndoa bila shaka nguvu za kiume zitaathirika."
Hufai kunywa maji mengi ya limau kwa wakati mmoja- Kitu chochote kikizidishwa huwa si kizuri lakini sio kibaya kwa wanandoa.


EmoticonEmoticon