Maafisa Wa Marekani Wadai Kushinikizwa Kuficha Ukweli Wa Ripoti Za Ujasusi Kuhusu Urusi

Afisa wa ngazi ya juu wa ujasusi katika wizara ya usalama wa ndani ya Marekani, amesema kuwa alishinikizwa na uongozi wa shirika la ujasusi kuficha tishio la Urusi la kuingilia uchaguzi kwasababu lingemfanya ''rais aonekane vibaya'' .

Mlalamishi aliyefichua taarifa hii, Brian Murphy alisema kuwa alishushwa cheo kwa kukataa kuzifanyia marekebisho ripoti juu ya suala hili na masuala mengine, ikiwa ni pamoja na suala la utawala wa wazungu.
Maagizo aliyopewa yalikuwa ni kinyume cha sheria, alidai.
Ikulu ya White House na Wizara ya usalama ya ndani imekanusha madai hayo. Mlalamishi aliachiliwa na kamati ya ujasusi ya bunge baadaye mwezi huu.


EmoticonEmoticon