Mabusu Bila Barakoa Yapigwa Marufuku

Boss mmoja wa ngazi ya juu kwenye idara ya Afya Nchini Canada Dr. Theresa Tam amepiga marufuku Wapenzi kupigana busu bila kuvaa barakoa (mask) wakiwa mahabani ili kukwepa kupata virusi vya corona.

"Kuna uwezekano mdogo wa kuambukizwa corona mkiwa mahabani, vya kuzingatia ni kuepuka kuzikutanisha nyuso zenu au hakikisheni kabla hamjazikutanisha nyuso zenu muwe mmezima midomo na pua kwa kuvaa mask na pia usisahau kuchunguza afya ya mpenzi wako kabla ya kukutana kimapenzi"

Mpaka September 1 2020 Canada ilikua na vifo vya Watu 9132 vilivyotokana na virusi vya corona huku Wagonjwa wakiwa zaidi ya laki moja na elfu ishirini ambapo hivi karibuni maambukizi yameripotiwa kupanda Nchini humo.


EmoticonEmoticon