Majaribio Ya chanjo Ya Covid-19 Kuanza Tena

Majaribio ya chanjo ya corona yameanzishwa tena baada ya zoezi hilo kusimamishwa kwa muda mfupi. 

Wakati huo huo idadi ya maambukizi inaendelea kuongezeka katika nchi kadhaa kote ulimwenguni. 

Matumaini ya kupata afueni kutokana na janga la corona duniani kote yalididimia mapema wiki hii wakati kampuni ya dawa ya AstraZeneca na Chuo Kikuu cha Oxford cha nchini Uingereza zilipotangaza kuwa zimesitisha majaribio ya chanjo hiyo baada ya mtu aliyejitolea kutoka Uingereza kupata ugonjwa ambao haueleweki.

Lakini hapo Jumamosi 12/09/2020 majaribioya chanjo hiyoyalipewa ruhusa ya kuanza tena na wasimamizi wa Uingereza baada ya chanjo hiyo kufanyiwa ukaguzi na kudhihirishwa kuwa ni salama. 

Kampuni ya dawa ya AstraZeneca pia imetangaza kwamba itaanza tena majaribio ya chanjo hiyo huko nchini Brazil baada ya kupewa ruhusa.
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya dawa ya AstraZeneca Tom Mc Killop.

Huku mamilioni ya watu wakiwabado wanakabiliwa na athari za maambukizi ya corona na ugonjwa wa COVID -19, mbio za kutafuta chanjo ulimwenguni kote  zinaendelea. Kampuni tisa tayari zikiwa katika awamu ya tatu ya majaribio ya chanjo ya corona.


EmoticonEmoticon