Maziwa Matatu Yaliojificha Yagunduliwa Katika Sayari Ya Mars

Maziwa matatu ya chini ya ardhi yamegunduliwa karibu na eneo la kusini mwa sayari ya Mars.

Wanasayansi pia wamethibitisha uwepo wa ziwa la nne - ambalo ishara za uwepo wake uligunduliwa 2018.

Maji ni muhimu kwa baiolojia, hivyobasi ugunduzi huo utakuwa muhimu kwa watafiti wanaotafuta uhai nje ya dunia.

Lakini maziwa hayo pia yamedaiwa kuwa na chumvi nyingi sana hali inayofanya kiumbe chochote kutoweza kuishi ndani yake.

Hali nyembemba ya hewa katika sayari ya Mars ina maana kwamba uwepo wa maji katika sakafu ya sayari huo upo chini . lakini maji yanaweza kuwepo chini ya ardhi yake.

Ugunduzi huo wa hivi karibuni ulifanyika kwa kutumia data kutoka kwa kifaa cha rada katika kituo cha angani cha bara Ulaya Esa ambacho kimekuwa kikizunguka katika sayari hiyo nyekundu tangu 2003. Mwaka 2018, watafiti walitumia data kutoka rada ya Mars ili kuripoti ishara za ziwa lenye ukubwa wa kilomita 20 ndani ya ardhi ya Mars .

Hatahivyo ugunduzi huo unatokana na tafiti 29 zilizofanywa na Marsis kati ya 2012 na 2015.


EmoticonEmoticon