Mazungumzo Kati Ya Pande Zinazozozana Afghanistan Yaanza Qatar

Mazungumzo ya amani kati ya Kundi la Taliban na serikali ya Afghanistan yalianza jana nchini Qatar katika kile waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo amekitaja kuwa ''ufanisi mkubwa'' katika miaka 19 ya vita. 

Wakati wa sherehe ya ufunguzi wa mkutano huo mjini Doha, wajumbe wa mazungumzo hayo walikiri kuwa mazungumzo hayo yatakuwa magumu na yenye fujo. 

Pompeo amekiri kuwa watakumbana na changamoto nyingi katika mazungo hayo katika siku zijazo, wiki na miezi na kutoa wito kwa pande zinazozozana kutumia fursa hiyo kupata amani. 


Pompeo aliziambia pande hizo zinazozozana kukumbuka kuwa maamuzi yao hayatakuwa ya kizazi cha sasa pekee lakini pia cha vizazi vijavyo. 

Wakati huo huo, kundi la Taliban jana liliwaachia huru wanajeshi 22 wa serikali ya Afghanistan kama ''hatua ya nia njema'' kuadhimisha mwanzo wa mazungumzo hayo.


EmoticonEmoticon