Mazungumzo Ya Kihistoria Ya Amani Kati Ya Afgha, Talban Yaanza

Mazungumzo ya kwanza ya amani kati ya serikali ya Afghanistani na Taliban yameanza Qatar, baada ya kucheleweshwa kwa miezi kadhaa.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo ameuita mkutano huo kuwa wa kihistoria wakati akielekea Doha katika sherehe za ufunguzi.
Mazungumzo hayo yalipaswa kuanza baada ya Marekani na Taliban kusaini mkataba wa amani mwezi Februari.
Lakini utata ulikuja katika hatua ya kukubali kubadilishana wafungwa , wakati vurugu huko Afghanistan iliyochukua miongo minne kuwa katika kumalizika.
Ujumbe wa raia wa Afghan kuondoka Kabul kuelekea Doha ulitolewa Ijumaa - 11 Septemba, miaka 19 shambulio baya la Marekani kutokea na kusababisha mwisho wa utawala wa Taliban.
Mkuu wa mazungumzo hayo bwana Abdullah Abdullah, alisema wanatafuta haki na amani.
Bwana Pompeo alizungumza katika mkutano kuwa anaamini kuwa Marekani italinda haki ya kila mtu nchini Afghanistan "Hii ni namna nzuri ya kusitisha ghasia na kwa manufaa ya kizazi hiki na kizazi kijacho".
Siku ya Alhamisi , Taliban ilithibitisha kuwa itahudhuria baada ya kundi la mwisho la wafungwa sita kuachiwa huru.
Katika mkutano kiongozi wa Taliban bwana Mullah Baradar Akhund ametaka Afghanistan kuwa na mfumo wa kiislamu ambao utakubalika katika jamii zote na kuwafanya watu waishi kwa upendo na kindugu.


EmoticonEmoticon