
Mfungwa aliyemshambulia mwimbaji wa RnB duniani, Robert
Kelly, maarufu R Kelly wakiwa
gererani amejitokeza na kuzungumza sababu hasa za kumshambulia mwimbaji huyo.
Mfungwa huyo aliyejitambulisha kwa jina
la Jeremiah
Shane Farmer (39) amesema alitumwa na serikali kufanya
shambulizi hilo la kumdhuru R Kelly,
“Serikali ilinifanya nimshambulie R. Kelly,”
alisema Jeremiah.
Kwa mujibu wa The Blast, Jeremiah, ametambulika
kuwa ni mmoja kati ya memba hatari wa kundi la kihalifu maarufu kama Latin
Kings.
Sambamba na hilo, Jeremiah alidai kuwa alifanya tukio hilo
kwa lengo la kupata umaarufu na dunia kufahamu kwamba serikali inanuka rushwa.
EmoticonEmoticon