Mkuu Wa Serikali Inayotambuliwa Na UN Kujiuzulu Libya

Waziri Mkuu wa serikali ya Libya inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa Fayez Serraj ametangaza nia ya kukabidhi madaraka kwa uongozi mpya mwezi Oktoba, wakati mazungumzo yakiendelea kusuluhisha mzozo nchini mwake.

''Natangaza nia yangu ya dhati ya kukabidhi hatamu za uongozi kwa baraza la utawala linalofuata, kabla ya mwezi Oktoba kumalizika'', ndivyo  alivyotangaza nia yake waziri mkuu Fayez Serraj katika hotuba kwa taifa lake kupitia televisheni usiku a kuamkia leo. 

Kiongozi  huyo amesema hali ya kisiasa na kijamii nchini Libya iko katika mivutano mikubwa, na hali hiyo inazitatiza juhudi za kutafuta suluhisho la kisiasa na kuepusha umwagikaji wa damu.


EmoticonEmoticon