Mmea Unaodaiwa Ni Dawa Ya Corona Madagaska

Madagascar iliwavutia wengi na kuangaziwa sana Aprili taifa hilo lilipotangaza kwamba lilikuwa limevumbua dawa ya corona kutoka kwa mmea.

Dawa hiyo iliyokuwa imeandaliwa kama kinywaji ilitengenezwa kwa kutumia mmea wa artemisia, na rais Andry Rajoelina aliipigia debe sana.
Kufikia sasa bado hakuna ushahidi kwamba mmea huo - ambao kemikali zake huweza kudhibiti malaria - unaweza kutibu Covid-19, kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO). 
Tunafahamu nini kufikia sasa kuhusu mmea huu na nguvu zake?
Mmea huo kwa jina kamili huitwa Artemisia annua na asili yake ni bara Asia, lakini hukuzwa katika maeneo mengi duniani yenye joto na jua.
Mmea huu umekuwa ukikuzwa katika baadhi ya mataifa ya Afrika mashariki zikiwemo Kenya na Tanzania.
Mmea huu umetumiwa kama tiba ya kiasili nchini China kwa zaidi ya miaka 2,000 kutibu magonjwa mengi, ukiwemo ugonjwa wa malaria. Hutumiwa pia kupunguza maumivu na kudhibiti homa.
Nchini Uchina, mmea huo hufahamika kama "qinghao."  
Kwa Kiingereza huitwa sweet wormwood au annual wormwood, na baadhi ya watu wamekuwa wakiutumia kwa sababu mbalimbali kama tiba, na hata kuongezwa kwenye vinywaji.


EmoticonEmoticon