Ndege Za Israel Zaupiga Ukanda Wa Gaza

Mashahidi wamesema kuwa ndege za kivita za Israel zimeushambulia Ukanda wa Gaza, na ving'ora vya tahadhari vimelia kusini mwa Israel, baada ya roketi kutoka Gaza kuanguka katika mji wa Israel wa Ashdod, Wakati Israel ilipokuwa ikisaini makubaliano ya kidiplomasia na Bahrain na Umoja wa Falme za Kiarabu mjini Washington. 

Watu wawili wamejeruhiwa na roketi hilo. Duru zimearifu kuwa mashambulizi ya ndege za Israel yalikilenga kituo cha mafunzo cha kundi la wanamgambo la Hamas linaloudhibiti Ukanda wa Gaza. 

Jeshi la Israel halijathibitisha mashambulizi hayo, lakini limesema ving'ora vimelia kuwaweka wakazi wa kusini mwa nchi hiyo katika hali ya tahadhari.


EmoticonEmoticon