Precision Air Yafuta Safari Ya Kuelekea Nairobi

Shirika la ndege Precison Air lenye makazi yake Tanzania limefuta mipango ya kuanza kwa safari za ndege kuelekea Nairobi baada ya serikali ya Kenya kusema kuwa haitafuta haki za usafiri za kampuni hiyo, wakati huu kukiwa na mvutano baina ya nchi hizo mbili, gazeti la Business Daily limeandika.

Taarifa iliyochapishwa kwenye ukurasa wake wa twitter, imesema inaahirisha mipango hiyo kwasababu ya idadi ndogo ya wateja wanaotaka kusafiri, ikiahidi kuwa tarehe nyingine ya safari kuelekea Nairobi itapangwa na kuchapishwa kwenye tovuti yao hivi karibuni.

Credit:Bbc


EmoticonEmoticon