Producer Scott Storch Alichomtabiria Chris Brown Chatimia

Mtayarishaji Scott Storch alimuahidi Chris Brown kwamba atakuwa msanii mkubwa na maarufu sana, hii ilikuwa kipindi ambacho Breezy anaanza muziki akiwa na umri wa miaka 16.

Baada ya kutembelea studio siku moja, Scott akiwa kwenye ubora wake akiwa tayari amefanya kazi na mastaa wakubwa wa dunia, alimpokea Chris Brown na kumwambia anaenda kubadilisha yake.

Storch alimrekodia Breezy wimbo wa "Run It" wimbo wa kwanza kwenye maisha yake ya muziki, ambao pia ulimpa mafanikio makubwa na kumtambulisha. Kabla ya kuanza kurekodi Storch alimwambia Breezy "Ninaenda kukutengenezea wimbo namba 1 na utakuwa msanii maarufu sana."

Wimbo huo 'Run It' ulitoka mwaka 2005 na uliandikwa na Sean Garrett pia Juelz Santana alishirikishwa. Baada ya miaka 15, leo Chris Brown ni miongoni mwa wasanii walioacha alama kubwa kwenye muziki duniani, akiweka rekodi nyingi na kushinda tuzo kibao.


EmoticonEmoticon