Raia Wa Iraq wauawa Katika Shambulio La Roketi

Raia watano wa Iraqi wameuawa baada ya roketi kurushwa kwenye nyumba iliyokuwa karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad, jeshi la Iraqi limesema.

Waathirika walikuwa wanawake wawili na watoto watatu kutoka kwa familia moja. Watoto wengine wawili walipata majeraha.
Hakuna kundi ambalo limedai kurusha roketi hiyo lakini uwanja wa ndege ikiwemo kambi ya jeshi ya Marekani, mara nyingi nyingi ndio inayolengwa na kulaumiwa wanamgambo wanaounga mkono Iran wanaopigwa na Marekani.
Hii ilikuwa mara ya kwanza katika kipindi cha miezi kadhaa raia wa kawaida kujeruhiwa.
Waziri Mkuu wa Iraqi Mustafa al-Kadhimi aliagiza kusimamishwa kazi kwa vikosi vya usalama katika uwanja wa ndege kufuatia ajali hiyo iliyotokea Jumatatu.
Maafisa watachukuliwa hatua kwa kushindwa kuchukua hatua na kuruhusu vitendo vya ukosefu wa usalama kama hivyo, taarifa hiyo imesema.
Bwana Kadhimi ametoa wito wa juhudi za pamoja"kumaliza uhalifu wa aina hiyo dhidi ya raia" na kuahidi kutoruhusu "magenge hayo kuwa huru wakati yanatatiza usalama bila ya kuadhibiwa".
Kushindwa kwa Serikali ya Iraqi kusitisha mashambulizi ya roketi yanayorushwa kuelekezwa uwanja wa ndege na uwanja wa ubalozi wa Marekani huko Baghdad kumesababisha wasiwasi mkubwa.


EmoticonEmoticon