Rais Wa Zamani Boubacar Keita Apelekwa Abu Dhabi Kwa Matibabu

Ibrahim Boubacar Keita
Afya ya kiongozi huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 75 imekuwa sio nzuri na kusababisha kulazwa hospitalini mara alipoachiwa baada ya kuzuiliwa na watawala wa kijeshi kwa siku 10. 

Duru za kidiplomasia nchini Mali zimesema Rais wa Mali aliyeondolewa madarakani kwenye mapinduzi ya kijeshi mnamo mwezi Agosti, Ibrahim Boubacar Keita,alisafirishwa mwishoni mwa wiki na kupelekwa Falme za Kiarabu kwenda kupata matibabu.

Kiongozi huyo wa Mali aliyeondolewa madarakani ameandamana na mkewe, Aminata Maiga Keita, msaidizi, madaktari wawili na maafisa wanne wa usalama, hayo ni kwa mujibu wa Mamadou Camara mkuu wa zamani wa wafanyikazi wa Bobackar Keita aliyeliambia shirika la habari la Reuters kuwa Keita aliondoka kutoka mjini Bamako.

Jumamosi jioni ndani ya ndege iliyokodishwa na Falme za Kiarabu kufuatia ombi kutoka kwa mamlaka ya Mali na Keita mwenyewe, ili aweze kwenda kutibiwa katika hospitali ya kijeshi katika mji wa Abu Dhabi. Camara amesema hiyo ni ziara ya matibabu itakayochukua muda wa kati ya siku 10 hadi 15.


EmoticonEmoticon