Raisi Wa Ufaransa Aishinikiza Lebanon Kuunda Haraka Serikali Mpya

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amerejea Lebanon, nchi ambayo ipo katikati ya mgogoro usio wa kawaida, kwa ziara ya siku mbili iliyosheheni shughuli nyingi na mazungumzo ya kisiasa yanayolenga kuipa ufumbuzi nchi hiyo.

Macron alitua jana usiku mjini Beirut lakini mkutano wake wa kwanza haukuwa na waziri mkuu mpya aliyeteuliwa saa chache kabla, wala wanasiasa wanaozozana wa nchi hiyo au wanaharakati wa mashirika ya kijamii. 

Macron badala yake aliamua kumuona mwanamuziki nambari moja wa kike nchini Lebanon, Fairouz, ambaye ni alama ya kitaifa na mmoja wa vigogo wa nadra sana nchini Lebanon wanaopendwa na kuheshimiwa kote nchini humo. 

Mwanamuziki huyo maarufu katika ulimwengu wa Kiarabu, sasa ana umri wa miaka 86 na hajaonekana hadharani katika miaka ya karibuni. Mkutano na Fairouz ni ishara ya kibinafsi ya Macron.


EmoticonEmoticon