Raisi Wa Ufaransa Akamilisha Ziara Lebanon Na Onyo Kwa Viongozi

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amewapa wanasiasa wa Lebanon hadi mwisho mwa mwezi Oktoba kuanza kutekeleza mageuzi, akisema msaada wa kifedha utazuiwa na baadaye kuwekewa vikwazo kama rushwa itazuia mchakato huo.

Macron ameuambia mkutano wa wanahabari mjini Beirut kuwa viongozi wa kisiasa wamekubali kuunda serikali ya wataalamu katika wiki mbili zijazo kusaidia kuliweka kwenye mkondo sahihi taifa hilo la Mashariki ya Kati linalozidiwa na uzito wa mporomoko wa kiuchumi.

Macron amesema Paris iko tayari kusaidia kuandaa na kuwa mwenyeji wa mkutano wa kimataifa na Umoja wa Mataifa mwezi Oktoba. 

Rais huyo wa Ufaransa amesema vikwazo huenda vikatangazwa kama kutakuwa na ushahidi wa rushwa na vitaratibiwa na Umoja wa Ulaya, lakini hiyo sio mada ya Oktoba kwa sababu kwa sasa wapo katika mchakato wa kuaminiana na kushirikiana.

 "Nilisema hiki wazi, kama ikifika Oktoba, na walichokiahidi viongozi wenu hakijafanyika, tutahitaji kufanya maamuzi. 

Hii inamaanisha nini? inamaanisha hakuna kilichofanyika, kwa hiyo nitahitaji kuifahamisha jamii ya kimataifa kuwa hatuwezi kutoa msaada wetu. 

Lakini pia nitahitaji kuwaeleza Walebanon kuwa tulikuwa tayari kusaidia lakini viongozi wenu wakaamua vinginevyo." Amesema Macron.


EmoticonEmoticon